Mkoa wa Mbeya
From Wikipedia
Mkoa wa Mbeya ni kati ya mikoa 26 ya Tanzania ikipakana na Zambia na Malawi, halafu na mikoa ya Rukwa, Tabora, Singida na Iringa.
Kuna wilaya 8 zifuatazo: Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini, Rungwe, Kyela, Ileje, Mbozi, Chunya na Mbarali.
Mbeya ni kati ya maeneo yanayopendeza kabisa ndani ya Tanzania ikiwa na sehemu za Ziwa la Nyasa, Ziwa Rukwa, milima ya Mbeya, milima ya Rungwe, Uwanja wa juu wa Uporoto, Uwanja wa Usangu ingawa haukufikiwa bado na utalii.
Wilaya ya Rungwe ni eneo penye mvua nyingi katika Tanzania. Mkoa wa ujumla ni mojawapo kati ya mikoa yenye kilimo kizuri inayotoa mazao ya kulisha taifa. Lakini maeneo makubwa ya Wilaya ya Chunya ni makavu.
Wilaya ya Chunya ina madini mbalimbali hasa dhahabu. Mbeya na Mbozi kahawa hupandwa. Rungwe pana chai nyingi, pamoja na Rungwe na Chimala hulimwa mpunga. Nyanda za juu kuna nafaka na viazi.
[edit] Maziwa na mito
Mkoa wa Mbeya inapakana na maziwa mawili makubwa ndiyo Ziwa Nyasa na Ziwa Rukwa. Hasa milima yenye asili ya volkeno ya wilaya ya Rungwe inyajaa maziwa ya kasoko.
Mito mikubwa ni Songwe na Kiwira. Chanzo ya mto Ruvuma iko pia Mbeya katika tambarare ya Usangu.
[edit] Viungo vya nje
en: MBEYA REGION SOCIO-ECONOMIC PROFILE [[1]]
|
|
---|---|
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |