Nile ya buluu
From Wikipedia
Mto wa Nile ya buluu (Ethiopia: Abbai) | |
---|---|
|
|
Chanzo | Ziwa Tana (chemchemi ya Gishe Abbai) |
Mdomo | Mto Nile mjini Khartum |
Nchi | Ethiopia, Sudan |
Urefu | 1.350 km |
Kimo cha chanzo | 1830 m |
Mkondo | ?? m³/s |
Eneo la beseni | 326,400 km² |
Nile ya buluu ni tawimto mkubwa wa mto Nile. Inaanza katika Ziwa Tana kwenye nyanda za juu za Ethiopia ikiitwa kwa jina la Abbai. Mdomo wake ni Sudan mjini Khartum inapounganika na Nile nyeupe.
Kwa jumla Nile ya bluu inabeba maji mengi kushinda Nile nyeupe.