Selman Waksman
From Wikipedia
Selman Abraham Waksman (22 Julai, 1888 – 16 Agosti, 1973) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Ukraine. Baadaye alihamia na kupata uraia wa Marekani (mwaka wa 1916). Hasa alichunguza vijiumbe vya ardhini na kugundua viua vijasumu. Mwaka wa 1952 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.