Bata-miti
From Wikipedia
Bata-miti | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Bata-miti uso-mweupe
|
||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Mabata-miti au Dendrocygninae ni familia ndogo ya familia Anatidae yenye jenasi moja tu, Dendrocygna. Waainishaji wengine wanawaweka ndani ya familia yao wenyewe Dendrocygnidae au ndani ya kabila Dendrocygnini ya familia ndogo Anserinae. Leo kuna spishi nane za mabata-miti na visukuku vya spishi ingine vimefunuliwa kisiwani kwa Aitutaki, Visiwa vya Cook. Wanaitwa mabata-miti kwa sababu hujenga matago yao pengine ndani ya miti. Lakini kwa Kiingereza wanaitwa “whistling ducks” sikuhizi kwa sababu ya sauti yao kama mluzi. Mabata hawa wanatokea popote kwa kanda za tropiki na nusu-tropiki. Wana miguu mirefu na shingo refu na wanapenda kuwa pamoja. Makundi makubwa ya ndege hawa huonekana maziwani.
[edit] Spishi za Afrika
- Dendrocygna autumnalis, Bata-miti Tumbo-jeusi (Black-bellied Whistling Duck)
- Dendrocygna bicolor, Bata-miti Kahawia (Fulvous Whistling Duck)
- Dendrocygna viduata, Bata-miti Uso-mweupe (White-faced Whistling Duck)
[edit] Spishi za mabara mengine
- Dendrocygna arborea (Black-billed Whistling Duck)
- Dendrocygna arcuata (Wandering Whistling Duck)
- Dendrocygna eytoni (Plumed Whistling Duck)
- Dendrocygna guttata (Spotted Whistling Duck)
- Dendrocygna javanica (Lesser Whistling Duck)