User:Kipala
From Wikipedia
Nina nywele lakini nimependa jina hili la Kipala. Nikiwa Mjerumani nimekaa miaka mingi Tanzania na Kenya. Hata nikihofia ya kwamba nimeanza kutumia Kiswahili cha Nairobi hapo na pale bado naona nitoe shukrani zangu kwa Afrika ya Mashariki kwa njia ya kusaidia kujenga Wikipedia ya Kiswahili. Basi jamani, kuna kazi, twendeni! --Kipala 21:11, 14 Januari 2006 (UTC)
- Kipala, asante sana kwa kunikaribisha. Kuhusu majina ya nchi, kuna orodha nzuri inayopatikana kwenye Kamusi Hai. Orodha hii inafuata orodha tatu nyingine: zile za BAKITA, TUKI, na Redio Tanzania Dar es Salaam. Vikundi hivi vitatu vilisanifisha (au viliswahilisha, ukipendelea) majina ya nchi zote za dunia. Kama ulivyosema, mara nyingi hakuna makubaliano baina ya vyanzo mbalimbali, na orodha hiyo ya Kamusi Hai inaonyesha mitafaruku. Lakini kwa jumla orodha ya Kamusi Hai inaonyesha majina yaliyopendekezwa na wataalamu wa vyuo na waandishi wa habari. Je, tufuate mapendekezo haya, au tuhimize istilahi nyingine ya Kiwikipedia? Nafikiri ni afadhali tufuate njia moja na wao waliopewa cheti kusanifisha lugha rasmi, lakini naomba shauri lako.
- Orodha ya TUKI ilichapishwa katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Toleo la Pili, mwaka 2004, kurasa 473-477. Orodha hii ilifuata mapendekezo rasmi ya orodha ya BAKITA kutoka mwaka 2001, lakini ilibadili maneno mbalimbali (Ekwado badala ya Ikwado, kwa mfano). Baada ya hapo, Redio Tanzania Dar es Salaam ilipendekeza mabadiliko mengine mwaka 2005, kufuatana na matumizi yao. Mapendekezo yote yanaonekana katika orodha ya majina ya nchi iliyoandaliwa na Kamusi Hai ya Kiswahili kwenye Mtandao. Malangali 18:04, 23 Juni 2006 (UTC)
Kipala, unakaribishwa kujiunga kwenye kikundi cha mazungumzo kuhusu mawikipedia ya lugha mbalimbali za Kiafrika. Naomba utembelee http://groups.yahoo.com/group/afrophonewikis/ kujiandiksha. Asante, Malangali 19:21, 16 Agosti 2006 (UTC)
Maswali magumu Kipala. Unaonaje nikiweka maswali haya pale kwenye kamusi hai mtandaoni? Binafsi ninapendelea "gamba" zaidi ya "ganda." Na "kiini" zaidi ya "masoka". Sioni ubaya kwenye kuazima neno na hivyo kutumia "manto." Unaonaje tukiuliza? --Ndesanjo
-
- Ni vizuri ukiuliza. Labda itavuta wengine katika mradi huu. "Koti" unaonaje? Vipi wazo la Templeti na maneno yake? --Kipala 21:51, 2 Septemba 2006 (UTC)
Kipala, nimejaribu kuweka jedwali kuhusu BBC lakini limekataa. Msaada? (ndesanjo)
-
- Samahani sijaelewa swali. Naona umehariri makala ya BBC. Tatizo ni nini? (kipala)
Nimeona sehemu mbalimbali (nje ya Wikipedia) zikitumia Jamhuri ya Kijerumani kama ilivyo kwenye Wikipedia. Kwanini isiwe Jamhuri ya Ujerumani? --Ndesanjo
-
- Ni swali la utafsiri. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani iliitwa "Deutsche Demokratische Republik" - ilitumia neno "deutsch" ambalo ni "kijerumani" likitaja tabia au pia lugha. Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani (Bundesrepublik Deutschland) linatumia neno "Deutschland" linalotaja nchi yenyewe. Kipala
Hello Kipala. Now that you are back, I would like to draw your attention to something which I find difficult to explain in Swahili. Have you noticed that since a while the lines that separate the sections of the articles are visible inside the taxoboxes? This is not the case in other Wikipedias. Can this be fixed? ChriKo 21:42, 13 Septemba 2006 (UTC)
-
- Saw the same. No idea. Pass it to admins --Kipala 22:30, 13 Septemba 2006 (UTC)
Naam kipala...
Hii ni kuonyesha ni jinsi gani nimefurahishawa na jinsi ulivyo hariri na kupangilia makala kuhusu Ubuddha. Kwa kweli imependeza!! Naomba uiangalie nyingine iliyopo kwenye majadiliano kuhusu Ukristo ningependa kuifupisha lakini kuna baadhi ya vielementi naona bado ni muhimu ukizingatia bado ninaiendeleza ili baadae ichujike. Hongera umechuje vizuri ile ya Ubuddha... Hii ya Ukristo naomba tusaidiane nayo ije kupendeza.
Upendo,
Moses
Kipala,
nashukuru kwa shauri lako... Ile makala ya "Ukristo" nadhani mbele nitaivunja kuwa Viungo tofauti vingi. Kwa mfano: Musa, Majia, majusi (Magic, Astrology), ilimu (esoteric), alikimu(alchemy), ginosia (gnosis), Agano la kale, Agano Jipya, Historia ya Kanisa, Nembo za kiilimu (esoteric seals and symbols), mafundisho, Kanisa zamani na sasa. Hivyo ninashauku ya makala nyingi. Labda na wewe umegundua sijamaliza; kwa kuwa nahitaji kwanza na makala ya mjadala kwani maneno mengi nimebuni mwenyewe na nitazidi kuyaleta. Kwa kweli inahitaji kutulia na wala sina haraka. Nikimaliza vipande vya sasa, nitasonga kwenye mambo ya sayansi. Naomba uendelee kufuatilia na kama utaanza kuona maana, ruhusa kuvunja makala na kutengeneza makala tofauti zenye kuingiliana.
Ahsante