Lugha ya kuundwa
From Wikipedia
Lugha ya kuundwa ni lugha ambayo msamiati na serufi zake zimetungwa na watu badala ya kukua kama sehemu ya utamaduni wa umma fulani. Kwa kawaida zinaundwa kwa ajili ya kuwasiliana kati ya watu sawasawa na lugha asilia. Nyingi zinatengenezwa ili kuwa lugha saidizi za kimataifa, lakini nyingine zinaundwa kwa ajili ya usiri au majaribio ya isimu au bila sababu fulani.
Lugha ya kuundwa inayozungumzwa zaidi ni Kiesperanto.
Mara chache lugha ya kuundwa maana yake ni lugha za kompyuta au za kuandaa programu (angalia lugha asilia). Kwa sababu ya utata huo watu wengi, hasa Waesperanto, hawapendi kutumia neno lugha ya kuundwa, na badala yake wanasema lugha ya kupangwa. Lakini msemo lugha ya kupangwa unatumika kwa lugha zile tu ambazo ziliungwa kwa ajili ya utumiaji wa kawaida baina ya watu.