Ngoma (muziki)
From Wikipedia
Ngoma inaoweza kumaanisha muziki unaochezwana na ala ya muziki inayoitwa ngoma pia.
Ngoma ni muziki na lugha ya pekee inayotumika kwa kuelezea utamaduni na historia ya nchi fulani, tunatumia lugha ya ngoma katika kuelezea hali mbalimbali za maisha yetu, kama vile huzuni, furaha, mapenzi, kutia moyo, vitisho, shukurani na ushindi.
Babu zetu walikuwa na lugha hii ya ngoma ambayo tumeirithi kwa mapokeo. Ngoma pia ilitumika na jamii mbalimbali kama njia ya kuita watu kwenye kusanyiko muhimu, kama vile vita, mikutano nk. ilipigwa kwa milio tofauti kulingana na tukio.