Nzige
From Wikipedia
Nzige ni jamii ya panzi wenye uwezo wa kujikusanya kwenye makundi makubwa na kuruka umbali mrefu kwa pamoja. Kuna aina nyingi ya nzige hususan nzige wekundu, nzige wa jangwani, nzige wasafiri, nzige kahawia, nzige wa mitini n.k.
Nzige wanapokuwa wametawanyika mmoja mmoja huishi kama panzi wa kawaida. Wanapozaliana na kuongezeka idadi hujikusanya katika makundi. Makundi ya tunutu husafiri kuelekea upande mmoja na kula majani wanakopitia. Makundi ya nzige wakubwa huweza kufikia idadi zaidi ya bilioni na huruka umbali mrefu na kuharibu mazao wanakotua.
Makala hiyo kuhusu "Nzige" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Nzige kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |