Ubaguzi wa rangi
From Wikipedia
Ubaguzi wa rangi ni kitendo cha kuthamini au kutenga binadamu kwa misingi ya rangi za ngozi. Ubaguzi wa rangi ulikuwa maarufu sana katika nchi kama Afrika Kusini na Marekani ambapo huko Waafrika walikandamizwa kutokana na rangi yao katika kupata huduma mbalimbali za kijamii na kimaendeleo.
Wakati wa ukoloni, rangi ilitumika kama msingi wa utoaji huduma muhimu mfano: shule, matibabu na haki nyingine za kibinadamu. Rangi nyeusi ilipewa hadhi ya chini zaidi.
Siku hizi katika karibu nchi zote, sheria zinapinga ubaguzi wa rangi. Lakini katika nchi nyingi bado kuna wabaguzi wachache ambao wanavunja sheria kwa kuendelea kubagua. Kwa mfano, kuna wabaguzi wanaobagua Watu weusi nchini Marekani na katika nchi za Ulaya.