Alpha Centauri
From Wikipedia
Alpha Centauri (pia: Toliman au Rigil Kentaurus) ni nyota inayong'aa sana katika anga ya kusini kwenye kundinyota ya Centaurus. Ni nyota ya kungaa sana ya nne angani lakini haionekani kwenye nusudunia ya kaskazini.
Alpha Centauri ni nyota ya pekee kwa sababu ni nyota yetu jirani katika anga ina umbali wa miaka ya nuru 4.2 - 4.2.
[edit] Mfumo wa nyota
Alpha Centauri ni sehemu ya mfumo wa nyota tatu. Nyota mapacha za Alpha Centauri A na Alpha Centauri B ziko miaka ya nuru 4.36 kutoka kwetu na nyota ya tatu Proxima Centauri ina umbali wa miaka ya nuru 4.22.