Anatolia
From Wikipedia
Anatolia (Kituruki: Anadolu) ni rasi kubwa katika Asia ya Magharibi kati ya Bahari ya Mediteranea na Bahari Nyeusi. Eneo lake ni sehemu kubwa ya Uturuki upande wa Asia.
Jina la Kale ni "Asia Minor" (kilat.)au " Asia ndogo".
Katika historia mataifa mengi yaliishi Anatolia na kujenga madola yao kama vile Wahitti, Wagiriki, Wajemi, [Waarmenia]], Waroma, Wagothi, Wabizanti na Waturuki.