Bishkek
From Wikipedia
Bishkek (Бишкек) ni mji mkuu wa Kirgizia. Ina wakazi 900,000 (2005).
[edit] Historia
Mji ulianzishwa kama kituo cha misafara kwenye barabara ya hariri kati ya China na Mashariki ya Kati. Khan wa Kokand alitengeneza hapa boma lililotwaliwa na jeshi la Urusi 1862 wakati wa uenezaji wa Urusi katika Asia ya Kati.
1878 Warusi walijenga mahali palepale kituo cha kijeshi kwa jina la "Pishpek" (Пишпек). Kituo kikakua haraka kuwa mji kwa sababu wakulima Warusi walipewa mashamba katika eneo hili.
Baada ya mapinduzi ya Urusi ya 1917 mji ulibadilishwa jina ukaitwa "Frunze" (Фрунзе) kwa heshima ya jemadari mkomunisti Mikhail Frunze.
Tangu kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti mwaka 1991 mji ukawa mji mkuu wa nchi mpya ya Kirgizia ikarudishwa jina la kale kwa umbo la "Bishkek".
Makala hiyo kuhusu "Bishkek" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Bishkek kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |