Bloemfontein
From Wikipedia
Bloemfontein (tamka: "Blumfontain" - Kiholanzi/Kiafrikaans "chemchemi ya maua") ni kati ya miji mikuu mitatu ya Afrika Kusini pamoja na Pretoria na Cape Town. Jina la Kisotho ni Mangaung linalomaanisha "kwa duma". Bloemfountain ni makao ya Mahakama Kuu ya Afrika Kusini pia mju mkuu wa mkoa wa Vrystaat (au: Free State - "Jamhuri huru").
Mji uko kwenye uwanja wa juu wenye kimo cha 1,395 m juu ya UB.
Mji mwenyewe una takriban wakazi 500,000. Kuna mji wa pili pamoja nao wa Mangaung wa wakazi 650,000 uliojengwa wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi kwa ajili ya watu weusi.