Bratislava
From Wikipedia
Bratislava ni mji mkuu wa Slovakia mwenye wakazi 450,000. Majina mengine ya kihistoria ya mji huu ilikuwa Pressburg (Kijerumani) au Pozsony (Kihungaria). Iko kando la mto Danubi.
Ishara ya mji ni boma la Bratislava lililosimama tangu karne za kati.
Contents |
[edit] Jiografia
Bratislava iko kwenye mpaka wa kusini-magharibi ya Slovakia karibu na Austria na Hungaria si mbali na mpaka wa Ucheki.
[edit] Historia
Eneo la mji lilikaliwa tangu milenia nyingi. Kiini cha mji wa leo kilikuwa boma la Bratislava lililojulikana tangu mwaka 805 BK.
Utawala wa eneo la mji ulibadilika mara kadhaa lakini tangu 907 mji ulikuwa sehemu ya ufalme wa Hungaria hadi mwaka 1918. Kati ya 1524 hadi 1830 ulikuwa mji mkuu wa Hungaria. Wakazi wake walikuwa hasa Wajerumani na Wahungaria pamoja na Waslovakia.
Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia eneo la mji liliingizwa katika nchi mpya ya Chekoslovakia jina likabadilishwa kuwa Bratislava. Mji ukawa mji mkuu wa sehemu ya Kislovakia ya nchi.
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na tena baada ya kuachana kwa Chekoslovakia mwaka 1993 Bratislava imekuwa mji mkuu wa Slovakia.
[edit] Biashara
Bratislava ni mji wa viwanda kuna viwanda vya motokaa, kemia, mashine na vifaa vya stima.
[edit] Usafiri
Mji ni njiapanda ya barabara kuu pia ya reli. Usafiri kwa maji hutumia bandari ya Bratislava kwenye mto Danubi. Kuna pia Uwanja wa Ndege wa kimataifa.
Usafiri wa mjini ni kwa mabasi, reli za barabarani na mabasi ya umeme.
[edit] Picha za Bratislava
[edit] External links
Template:Commonscat