Bujumbura
From Wikipedia
Bujumbura, ni Mji Mkuu wa Burundi unaokadiriwa kuwa na idadi ya wakazi 300,000. Mji huu upo kaskazini mashariki mwa Ziwa Tanganyika, na ni mji mkubwa zaidi Burundi, kitovu cha mawasiliano na uchumi nchini humo. Bujumbura ni mji pekee Burundi ambao una bandari ya kupakia mali na bidhaa mbalimbali za kuuza nje. Bidhaa kama kahawa, pamba, ngozi, na madini ya stani. Kwa kijiographia Bujumbura iko 3°22'34" Kusini, 29°21'36" Mashariki (-3.3761111, 29.36) [1].
Bujumbura ilipanuka toka ilipokuwa kijiji kidogo kilichokuwa kambi ya Jeshi ya Wajerumani. Eneo hii iliitwa Afrika ya Mashariki ya Ujerumani mwaka wa 1889. Lakini, baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Bujumbura ilichukuliwa na Ubeljiji ambapo Ligi ya Kimataifa ilisimamia Ruanda-Urundi. Jina la mji likabadilishwa kutoka Usumbura hadi Bujumbura Burundi ilipopata uhuru, mwaka wa 1962. Bujumbura ni mji ambao umeshuhudia vita vya ukabila kati ya Wahutu na Watutsi kwa kung'ang'ania Uongozi wa Burundi.
Kati ya mji huu kuna majengo ni yale ya kikoloni na pia kuna soko, uwanja wa taifa, mskiti mkubwa na kathidro. Pia kuna Jumba la Makumbusho ambalo linaitwa jumba la makumbusho ya maisha na jumba la makumbusho ya Jiologia. Mambo mengine ya kuchangamsha ni kama Hifadhi ya Rusizi, na Kiamba hapo Mugere, ambapo panasemekana kwamba David Livingstone na Henry Stanley walikutana. (Lakini watu wengi wasema walikutana Ujiji), Kigoma, nchini Tanzania ambapo panasemekana ni mwanzo wa mto ulio unaosemekana kuwa hapo ndio mwanzo wa Mto Nile.