Elias Canetti
From Wikipedia
Elias Canetti (25 Julai, 1905 – 14 Agosti, 1994) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Bulgaria. Baadaye aliishi nchini Uingereza. Aliandika riwaya na pia tamthiliya; aliandika maandishi yake yote katika lugha ya Kijerumani. Mwaka wa 1981 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.