Emilio Segre
From Wikipedia
Emilio Segre (1 Februari, 1905 – 22 Aprili, 1989) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Italia. Mwaka wa 1938 alihamia Marekani. Hasa alifanya utafiti wa fizikia ya kiini. Mwaka wa 1959, pamoja na Owen Chamberlain alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.