Hendrik Antoon Lorentz
From Wikipedia
Hendrik Antoon Lorentz (18 Julai, 1853 – 4 Februari, 1928) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uholanzi. Alitafiti nadharia ya elektroni. Pia alichunguza nadharia ya Albert Einstein (Relativity Theory) na ya kwanta. Mwaka wa 1902, pamoja na Pieter Zeeman alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.