Hori ya Chesapeake
From Wikipedia
Hori ya Chesapeake (Kiing.: Chesapeake Bay) ni hori la Atlantiki na pia mdomo wa pamoja wa mito kadhaa hasa mto Susquehanna. Imepakana na majimbo ya Virginia na Maryland.
Eneo lake ni 12,000 km² na inapokea maji ya beseni za mito inyoishia humo zenye jumla ya 165,800 km². Kijiolojia hori ni mwendo wa kale wa mto Susquehanna uliochimbwa miaka 15,000 iliyopita wakati wa enzi ya barafu ambako uwiano wa bahari ulikuwa mita 100 chini ya uwiano wa leo. Baada ya kupanda kwa uso wa bahari maji yake yalijaa bonde la mto na kulifanya kuwa hori la Atlantiki.
Sehemu nyembamba ya hori iko karibu na mji wa Annapolis (Maryland) penye daraja la Bay Bridge. Karibu na mdomo kuna handaki chini ya ardhi na chini ya bahari inayounganisha barabara pande zote mbili.
[edit] Mito inayoishia horini
- mto Susquehanna
- mto Potomac
- mto James (Virginia)
- mto Appomattox
[edit] Historia
Hori lilikuwa mahali pa mapigano kati ya manowari wa Ufaransa na Uingereza mwaka 1781. Wafaransa walizuia jeshi la Uingereza lisiongeze wanajeshi kutoka manowari zake likasaidia Wamarekani kushinda vita ya uhuru.