Irving Langmuir
From Wikipedia
Irving Langmuir (31 Januari, 1881 – 18 Agosti, 1957) alikuwa mwanafizikia na mwanakemia kutoka nchi ya Marekani. Alifanya utafiti kuhusu taa za gesi, neli za elektroni na vivuta hewa. Mwaka wa 1932 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia.