James Michener
From Wikipedia
James Albert Michener (3 Februari, 1907 – 16 Oktoba, 1997) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Marekani. Aliandika hasa riwaya zinazoeleza historia ya nchi au eneo la dunia. Mwaka wa 1948 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer kwa ajili ya mkusanyiko wake “Hadithi za Pasifiki ya Kusini” (kwa Kiingereza: Tales of the South Pacific) iliyoandikwa mwaka wa 1947.