Wikipedia:Jamii
From Wikipedia
English | Kiswahili | Francais | Deutsch (+/-)
Contents |
[edit] Uhamasishaji/Utangazaji
Malengo:
- Kutengeneza kamusi elezo kubwa ya Kiswahili itakayotumiwa na mtu yeyote bila gharama
- Kutafuta matumizi ya kamusi elezo hii mashuleni na kwenye miradi mbalimbali ya kielimu; kutumia yaliyomo ndani ya kamusi elezo hii (ambayo inapatikana kwa lugha mbalimbali)kwa faida za wazungumzaji wa Kiswahili na wale wanaojifunza Kiswahili
- Kushirikiana na wanafunzi wa vyuo vikuu na walimu wa lugha kuchangia na kuendeleza matumizi na mchango wa kazi hii
Kinachotakiwa:
- Orodha ya watu watakaojitolea,
- Orodha ya wanafunzi wenye hamu ya kushiriki,
- Orodha ya walimu wenye nia ya kushiriki na programu muafaka za kielimu
- makala fupi za msingi za maarifa duniani
[edit] Watu wenye nia ya kushiriki
- Ndesanjo
- Sj (Boston)
- Jeff (Toronto)
- Mshairi (Uingereza)
- Richard Mabala (Ethiopia/Tanzania)
- Joseph Tungaraza(Oz)
- Makene (Texas)
- Stan (Revolución) kutoka Florida
- maitha (kenya)
- Zablon Mgonja(Mtanzania) Chuo kikuu cha FISK marekani
- Matt Crypto (UK)
Walimu na wanafunzi
- Chuo Kikuu cha Nairobi
- Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam
- Shule za sekondari
- Kwingineko wanakofundisha lugha
Wanablogu wa Kiswahili na wataalamu wa teknolojia ya kompyuta
- Wanablogu wa Kenya naTanzania
- Uhamasishaji wa mdomo kupitia watu mbalimbali kama Ory, Ndesanjo, Jeff, Joseph, Nkya, Maitha, n.k.
[edit] Mambo ya awali ya kuweka kwenye kamusi elezo
Orodha ndefu: makala fupi za msingi za maarifa duniani; tuanze na makala 1000.
- Makala zilizoko kwenye kamusi elezo za Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, n.k. zinaweza kusaidia wanaoshiriki kuandika makala za awali za Kiswahili
Orodha fupi:
- Orodha ya Waafrika mashuhuri
- Wanasiasa: Wanasiasa wa mataifa ya Afrika
- Wasanii na waaandishi wa vitabu:
Mapendekezo ya mambo mengine ya kujumuisha katika kamusi elezo hii yanakaribishwa.
[edit] Mikutano ijayo
Kawaida mikutano hufanyika kupitia teknolojia ya IRC
Mkutano ujao utafanyika jumamosi ya tarehe kwanza, Oktoba, 2005. Saa: Itatangazwa baadaye
Malengo ya kutimiza kabla ya mkutano ujao:
#1: kuongeza idadi ya washiriki katika mkutano ujao #2: kuongeza idadi ya watu watakaoshiriki kuhariri kamusi elezo hii #3: kutafsriri ukurasa wa wikipedia:jamii #4: kuweka viunganishi vya makala au mambo yanayohusiana ndani ya makala mbalimbali za Kiswahili
[edit] Maoni
Tafadhali weka maoni na mawazo yako katika ukurasa wa mazungumzo. Sj