Jay Rosen
From Wikipedia
Jay Rosen (amezaliwa 5 Mei, 1956, Buffalo, New York) ni mwandishi na mwalimu wa uandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha New York. Jay Rosen anajihusisha kwa karibu na masuala ya Uandishi wa Raia. Kitabu chake kiitwacho What Are Journalists For? kilichotolewa mwaka 1996 kinazungumzia juu ya umuhimu wa kutumia zana mpya za habari kwa ajili ya mawasiliano na masikilizano.
Jay anaandika katika blogu yake iitwayo Pressthink ambayo inazungumzia juu ya taaluma ya uandishi katika zama za Intaneti. Pia huwa anaandika katika blogu ya The Huffington Post. Pressthink ilishinda tuzo ya Freedom Blog Award inayotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Reporters Withouth Borders mwaka 2005.