Jenerali
From Wikipedia
Jenerali ni cheo kikuu cha kijeshi katika nchi nyingi za dunia. Jenerali huwa ni kiongozi wa ngazi ya juu katika jeshi.
Idadi ya majenerali si kubwa. Kazi yao ni kuongoza na kupanga kazi ya jeshi. Kwa kawaida hawashiriki wenyewe katika mapigano.
Neno limeingia katika Kiswahili kutoka lugha ya Kiingereza. Asili yake ni Kilatini "generalis" yenye maana "kwa ujumla".
Categories: Jeshi | Cheo