John Enders
From Wikipedia
John Franklin Enders (10 Februari, 1897 – 8 Septemba, 1985) alikuwa daktari kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza virusi visababishavyo magonjwa mbalimbali. Mwaka wa 1954, pamoja na Frederick Robbins na Thomas Weller alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.