José Echegaray y Eizaguirre
From Wikipedia
José Echegaray y Eizaguirre (19 Aprili, 1832 – 4 Septemba, 1916) alikuwa mwanahisabati, mwanasiasa na mwandishi wa tamthiliya kutoka nchi ya Hispania. Alianza kuandika tu alipofikisha umri wa miaka 42. Kabla ya kuwa mashuhuri kama mwandishi, alikuwa profesa wa hisabati na mwanasiasa (kwa mfano, aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha mwaka wa 1874). Mwaka wa 1904, pamoja na Frederic Mistral alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.