Jostein Gaarder
From Wikipedia
Jostein Gaarder (amezaliwa 8 Agosti, 1952) ni mwandishi kutoka nchi ya Norwei. Alisoma falsafa, teolojia na masomo ya fasihi chuoni na kuwa mwalimu wa falsafa kabla hajajitegemea kama mwandishi. Ameandika hasa kwa watoto. Baadhi ya vitabu vyake ni:
- Ulimwengu wa Sofia (1991, kwa Kinorwei "Sofies verden")
- Siri ya Krismasi (1992, kwa Kinorwei "Julemysteriet")