Kisumu
From Wikipedia
Kisumu ni mji mkuu wa Mkoa wa Nyanza nchini Kenya mwenye wakazi 322,724 (1999). Ni mku mkubwa wa tatu wa Kenya pia mji mkubwa wa Kenya ya Magharibi na makao makuu ya wilaya ya Kisumu.
Mji uko kando la ziwa Viktoria Nyanza una bandari kubwa ya nchi kwa ziwa hilo. Mji na bandari vilianzishwa kwa jina la "Port Florence" mwaka 1901 wakati reli ya Uganda ilipofika hapa kutoka Mombasa.
Kuna feri ziwani kutoka Kisumu kwenda Mwanza, Bukoba, Entebbe, Port Bell na Jinja.
Kiuchumi Kisumu ina viwanda kadhaa hasa za sukari, samaki na vitambaa pia ya bia.
Maendeleo ya Kisumu yalikwama miaka mingi kwa sababu Waluo walisimama upande wa upinzani wa kisiasa kwa miaka mingi na serikali haikupeleka miradi tena katika mkoa huu.
Makala hiyo kuhusu "Kisumu" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kisumu kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |