Lev Landau
From Wikipedia
Lev Davidovich Landau (22 Januari, 1908 – 1 Aprili, 1968) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Urusi. Alichunguza vipengele vingi vya fizikia, hasa upande wa atomu, nyota, halijoto chini na kadhalika. Mwaka wa 1962 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.