Magma
From Wikipedia
Magma ni mwamba ulioyeyuka kutokana joto kali na shindikizo ulio chini ya ardhi. Kimsingi ni kama lava inayopatikana juu ya ardhi.
Magma hukunsayika mahali pamoja ndani ya tabakamwamba ya ganda la dunia au katika tabakalaini ya koti. Mahali pale huitwa "chumba cha magma". Joto la chumba huelekea kuyeyusha mwamba imara juu yake na kusababisha kutokea kwa volkeno. Voleno nyingi ziko juu ya vyumba hivi vya magma ndani ya ganda la dunia.
Magma ni katika hali ya kiowevu ikiwa na halijoto kati ya 600 C° na 1600 C°, kwa kawaida kati ya 700°C na 1250°C.
Kuna aina mbalimbali za magma zinazotofautiana kikemia. Zinakuwa aina mbalimbali za mwamba.
Makala hiyo kuhusu "Magma" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Magma kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Categories: Mbegu | Jiolojia | Gandunia | Volkeno