Malindi
From Wikipedia
Malindi ni mji wa Kenya kwenye pwani la Bahari Hindi. Iko takriban 100 km kaskazini ya Mombasa kwa mdomo wa mto Galana.
Idadi ya wakazi ni takriban 117,000 ni makao makuu ya wilaya ya Malindi. Mji ni kitovu muhimu wa utalii kwenye pwani la Kenya.
Contents |
[edit] Historia
Malindi ni kati ya miji ya kale ya Waswahili. Mji umejulikana kuwepo tangu karne ya 13 BK kwenye mwambao uliojulikana kama "Azania" tangu zamani za Waroma na Wagiriki wa Kale. Kwa karne nyingi Malindi ilikuwa dola-mji muhimu wa Uswahilini ulioshindana na Mombasa juu ya kipaumbele kwenye pwani la Afrika ya Mashariki.
[edit] Wachina katika Malindi
Malindi ya karne ya 14 iliona ziara za wageni wawili kutoka mbali :
Mnamo 1414 jahazi za mpelelezi Mchina Zheng He zilifika Malindi. Sultani wa Malindi aliamua kumtuma balozi wa pekee pamoja na zawadi ya twiga kwenye meli hizi kwenda Nanking mji mkuu wa China. 1419 Wachina walirudi na kuwarudishwa mabalozi. Lakini ziara hizi hazikuleta mawasiliano ya kudumu kwa sababu China iliamua kidogo baadaye kuacha safari za upelelezi.
[edit] Vasco da Gama na kuja kwa Wareno
Mwaka 1498 Mreno Vasco da Gama alifika Malindi kutoka kusini katika safari yake ya kwanza ya kuelekea Bara Hindi. Wareno walikuwa watangulizi wa mataifa mengine ya Ulaya ya kutafuta njia ya Uhindi kwa sababu walitafuta faida ya biashara ya moja kwa moja iliyokuwa imebaki mkononi wa wafanyabiashara Waislamu waliowahi kutawala biashara kati ya Ulaya na Asia.
Vasco da Gama alipatana ushirikiano na sultani wa Malindi ulioendelea mpaka mwisho wa kuwepo kwa Wareno Uswahilini. Alipewa nahodha ya kumwongoza hadi Bara Hindi akajenga nguzo ya kumbukumbu unaosimama hadi leo karibu na bandari ya wavuwi Malindi.
Wareno walihamisha kituo chao kutoka Malindi kwenda Mombada 1593 walipojenga huko boma la Yesu. Katika Uswahili mpya baada ya kufukuzwa kwa Wareno tangu 1693 umuhimu wa Malindi uliendelea kushuka na mnamo mwaka 1800 ilikuwa mahali pa pori na maghofu tun.
[edit] Utawala wa Zanzibar
Utawala wa Usultani wa Zanzibar ulifufusha mji. Familia makabaila kutoka kisiwa na kutoka Omani walipewa ardhi karibu na Malindi wakaanza kujenga nyumba upya na kulima mashamba ya mazao ya soko kama pamba kwa kazi ya watumwa.
[edit] =Utawala wa Uingereza
Tangu 1888 pwani Malindi pamoja na pwani la Kenya zilikodishwa na Zanzibar kwa Uingereza na kuondoka katika utawala wa Sultani.
Kupigwa marufuku kwa utumwa wakati wa Kiingereza ulisababisha kukwama kwa mashamba makubwa na kurrudi nyuma tena kwa mji. Waingereza waliweka hapa kituo cha Mkuu wa Wilaya.
[edit] Utalii
Polepole mwambao mzuri wa Malindi umepata sifa kama mahali pa kupumzika kati ya Waingereza tangu miaka ya 1920. Hasa nafasi nzuri ya kuvua samaki kubwa ilivuta watalii wenye pesa kama Ernest Hemingway. Hapo mwanzo wa utalii wa Malindi.
Katika jamhuri ya Kenya utalii ilikuwa hasa Waitalia wamependa Malindi na kununua nyumba na kujenga mahoteli hapa.
Makala hiyo kuhusu "Malindi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Malindi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |