Margaret Clitherow
From Wikipedia
Margaret Clitherow (1556 – 25 Machi, 1586) alikuwa Mwingereza aliyebadilisha imani yake kutoka Kanisa la Anglikana kuingia Kanisa la Kikatoliki. Kwa vile aliwaficha mapadre nyumbani kwake na kuhudhuria misa ya kikatoliki, alishtakiwa mahakamani na kuuawa. Mwaka wa 1970 alitangazwa kuwa mtakatifu. Sikukuu yake ni 25 Machi.