Msaada wa kuanzisha makala
From Wikipedia
Ukitaka kubadili, kusahihisha au kuhariri makala, ubonyeze "hariri" kule juu katika ukurasa wowote.
Contents |
[edit] Viungo
Usiandike makala bila viungo, kwa sababu bila hivi maandishi yako hayatapatikana kwa mtu yeyote yatabaki siri yako tu!
Njia rahisi ya kuanzisha ni kutumia viungo vilivyopo bila makala. Haya yanaonekana kwa rangi nyekundu. Ukiona neno lenye rangi nyekundu maana yake ni ya kwamba mwandishi aliona inafaa kueleza jambo lile lakini hakuna makala bado. Ukibonyeza hapo utafungua ukurasa mpya na unaweza kuanza kuandika!
Ukitaka kuanzisha makala mpya kabisa, utengeneze kwanza kiungo kwa makala hiyo kutoka ukurasa mwingine kwa kutumia mabano mraba: [[ na ]]. Kwa mfano, ukitaka kuanzisha ukurasa kuhusu Kijerumani, andika [[Kijerumani]] katika makala ya lugha (katika sehemu ya "kurasa zinazohusiana"). Baadaye, ubonyeze kiungo hicho, na uandike makala.
Ukitaka kujua ufanye nini ili kusaidia kuboresha kamusi elezo hii, angalia Ukurasa wa jumuia.
[edit] Mpangilio wa makala
Makala ndefu bila mpangilio haivuti. Inasaidia sana ukiingiza vichwa. Hii ni rahisi! Utumie alama za = mbele na nyuma ya mstari wa kichwa.
==Kichwa kikubwa==
===Kichwa kidogo===
[edit] Picha
Ukitaka kutumia picha iliyopo katika Wikipedia ya lugha nyingine kuna njia mbili:
[edit] 1. Picha iko tayari katika wikipedia commons au katika sw.wikipedia
Hii ni jambo la kujaribu! Fungua makala katika lugha nyingine yenye picha inayotakiwa, bonyeza "edit", nakili yote pamoja na mabano.
Kwa mfano: [[Image:Europe CD 3 036.jpg|right|300px|thumb|View over Paris from the Eiffel Tower]])
Hapo unahitaji kubadilisha Maelezo ambayo ni maneno ya mwisho kati ya | na ]]. Andika elezo kwa Kiswahili kwa mfano "Paris inayvoonekana kutoka mnara wa Eifel". Ukitaka kubadilisha ukubwa unabadilisha namba mbele ya "px". 200 px itakuwa ndogo zaidi, 100 px ndogo sana, 400 px kubwa zaidi - wakati mwingine tayari kubwa mno. Jaribu kwa kubonyeza hapo chini kabisa "Mandhari ya mabadilisho". Ukiona picha - sawa. Usipoona picha: haipo mahali inapopatikana. Jaribu nyjia ya pili!
[edit] 2. Picha inachukuliwa kupitia kompyuta yako
a) hifadhi picha kwenye kompyuta unayotumia (kwa muda tu - baada ya kupakia unaweza kuifuta mara moja).
b) Jiandikishe kwa jina lako katika wikipedia ya Kiswahili. (bofya juu kulia, andika jina unalotumia)
c) chini kushoto utapata kiungo kinachoitwa "Pakia faili" (chini ya andiko "vifaa"). Bofya kiungo hicho.
d) Katika ukarasa ujao, unabofya kando la dirisha ndogo "Search" na kuteua faili ya picha kwenye kompyuta yako. Kwenye "summary" pakia anwani ya picha kwa mfano "http://en.wikipedia.org/wiki/Image:Europe_CD_3_036.jpg" kwa picha ya Paris. Halafu bofya "Upload file", na picha itakuwemo Wikipedia ya Kiswahili.
Unaweza kutumia picha kwa kuandika [[Image:jina_la_picha.jpg]].
[edit] Kuelekeza
Mara nyingi inatokea kwamba majina mawili yanafaa kwa makala fulani. Ikiwa hivi, lazima tuamue makala ipatikane chini ya jina gani. Lakini tunaweza kuelekeza kutoka jina jingine kwa jina sahihi la makala, ili watu waipate makala rahisi zaidi.
Ili kuelekeza kutoka jina moja kwenda jina sahihi la makala, tumia
- #REDIRECT[[Jina la makala]]
Unaweza kuangalia mfano huu: Abunuwasi.
[edit] Jamii au Category
Usisahau kuunganisha makala yako na jamii au category. Jamii ni kama orodha ya makala zote chini ya kichwa fulani.
Kwa mfano makala zote kuhusu nchi za Afrika zimeorodheshwa katika jamii "[[Category:Nchi za Afrika]]". Tafuta jamii inayoweza kufaa (tazama ukurasa wa Mwanzo). Wengine watasaidia kupanga makala yako ikionekana jamii nyingine inafaa zaidi.