Mshtarii
From Wikipedia
Mshtarii (kutokana na Kiarabu "المشتري" al-mshtari) ni sayari ya tano toka kwenye jua katika Mfumo wa jua na sayari zake.
Mshtarii ni sayari kubwa kabisa ya jua letu. Mada yake inazidi mara mbili na nusu mada ya sayari zote nyingine.
[edit] Angahewa
Uso wa sayari haionekani kwa sababu angahewa nzito inafunika kila sehemu. Mada ya angahewa ni hasa hidrojeni na heli. Kutokana na uzito wa angahewa shindikizo ndani yake inaongezeka sana katika vilindi vyake na kusababisha gesi za angahewa kuingia katika hali ya giligili (majimaji) inayobadilika kuwa mango (imara) ndani zaidi. Zamani iliaminika ya kwamba sayari yenyewe ni ya gesi iliyoganda lakini siku hizi wataalamu wa falaki huamini ya kwamba kuna kiini cha mwamba au metali.
Doa nyekundu inayoonekana usoni wa angahewa ni dhoruba ya tufani kubwa sana iliyotazamiwa mara ya kwanza miaka 300 iliyopita wakati darubini za kwanza zilipopatikana. Duniani tufani zinapotea kwa kawaida baada ya wiki kadhaa lakini doa nyekundu imeendelea bila kusimama.
[edit] Miezi
Mshtarii ina miezi 63 zilizotambuliwa hadi mwaka 2005. Ukubwa wa Io unakaribia kipenyo cha Utaridi ukipita kile cha Pluto. Mwezi mdogo kabisa wa Mshtarii unajulikana kwa namba tu una kipenyo cha 1 km.
Miezi minne mikubwa ilitambuliwa mwaka 1610 na Galileo Galilei aliyekuwa kati ya wanafalaki wa kwanza waliotumia darubini. Ndiyo Io, Europa, Ganymedi na Kallisto.
Makala hiyo kuhusu "Mshtarii" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Mshtarii kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Mfumo wa jua na sayari zake |
---|
Jua - Utaridi - Zuhura - Dunia (Mwezi) - Meriki - Mshtarii - Zohari - Uranus - Neptun |