New Delhi
From Wikipedia
New Delhi (Kihindi:|नई दिल्ली, Kiurdu: نئی دلی) ni mji mkuu wa Uhindi. Ina wakazi zaidi ya milioni kumi. Iko katika kaskazini ya nchi kwenye kingo za mto Yamuna katika tambarare ya bonde la Ganga. Kimo cha mji kipo 216 m juu ya UB kwa wastani.
Delhi ina historia ndefu sana iliyoanza mnamo mwaka 1200 KK. Iliharibiwa mara nyingi na kujengwa upya na kubadilisha jina pamoja na wakazi na watawala wake. Katika karne ziliyopita ilikuwa mji mkuu wa Dola la Moghul na tangu 1911 wa Uhindi wa Kiingereza.
Delhi Mpya au New Delhi ilianzishwa baada ya azimio la George V mfalme wa Uingereza na Kaisari wa Uhindi la kuhamisha mji mkuu kutoka Kalkutta kwenda Delhi. Mji mpya ulijengwa kando ya Delhi ya Kale na kukabidhiwa mwaka 1931. Ulisanifiwa na wasanifu Waingereza Edwin Lutyens (1869-1944) na Herbert Baker (1862-1946).
Tangu mwaka 1947 New Delhi ni mji mkuu wa Uhindi huru.