Pluto
From Wikipedia
Pluto ni sayari kibete inayozunguka jua ng'ambo ya Neptun. Mada yake ni mwamba na barafu. Kipenyo chake ni 2,390 km. Katika mwendo wake inakata njia ya Neptun kwa sababu njia yake ina umbo la duaradufu kali.
[edit] Miezi
Pluto ina miezi mitatu inayoitwa Charon, Nix na Hydra. Charon ni kama nusu ukubwa wa Pluto na umbali wa wastani ni 19,410 km. Nix na Hydra ni miezi midogo (kipenyo cha 45 na 160 km) yenye umbali wa 44,000 km kutoka Pluto.
[edit] Sayari au sayari kibete?
Pluto Ilikuwa ikitambulika kama sayari ya tisa katika mfumo wa jua na sayari zake toka mwaka 1930 hadi Agosti 2006. Vipimo vipya vilileta wasiwasi juu ya swali: Je, sayari ni kitu gani?, hasa baada ya kugundua magimba ya ziada nje ya Pluto yanayokaribia ukubwa wake lakini hayafai kuitwa sayari.
Umoja wa kimataifa wa wanafalaki uliondoa Pluto katika orodha ya sayari kwenye mkutano wake wa mwaka wa 2006. Badala yake wameiita sayari kibete. Hata hivyo baadhi ya wanasayansi wa falaki wamepinga uamuzi huo na wameanzisha kampeni ya kurekebisha uamuzi huo.
[edit] Viungo vya nje
- Tovuti ya kampeni ya kupinga Pluto kuitwa sayari mbilikimo
- Habari kuhusu wanasayansi wanaotaka Pluto iendelee kutambuliwa kama sayari
- Habari kuhusu Pluto kuondolewa kwenye orodha ya sayari
- Tovuti ya International Astronomical Union
Makala hiyo kuhusu "Pluto" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Pluto kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |