Pyonyang
From Wikipedia
Pyongyang (Kikorea: 평양 직할시 'Phyŏngyang chighalshi' kwa mwandiko wa Kilatini) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Korea Kaskazini mwenye wakazi 2,926,443 na pamoja na rundiko la mji watu 3,702,757 (2005). Ni kati ya mahali pachache ambako wageni wa nje wanaruhusiwa kutembelea.
Mji uko kwenye kusini-magharibi ya nchi karibu na mpaka na Korea ya Kusini. Pyonyang ni kitovu cha kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi cha nchi.
[edit] Historia
Pyongyang ni mji wa kale kwenye rasi ya Korea. Kuna hakika ya kwamba kituo cha biashara ya Kichina kiliundwa karibu na mji uliokuwepo tayari. 427 ilitajwa mara ya kwanza kama mji mkuu wa ufalme.
Mji ulivamiwa na Wajapani kati ya 1592 hadi 1593 halafu na China 1627. Katika karne ya 19 wamisionari wengi walifika Pyonyang waliojenga zaidi ya makanisa 100. Idadi ya wakristo iliongezeka hadi kufikia theluthi moja ya wakazi kabla ya Ukomunisti kuchukua serikali lakini imepungua baadaye kama dini zote.
Mji uliharibiwa vibaya katika vita ya Japani dhidi ya China ya 1894–1895. Chini ya utawala wa Japani kati ya 1910 hadi 1945 viwanda vingi vilijengwa.
Vita ya Korea ya 1950–1953 ilileta tena uharibifu mwingi. Baadaye mji ulijengwa upya kwa muundo wa miji ya Umoja wa Kisovyeti pamoja na bustani kubwa na barabara pana.
[edit] Hali ya maisha
Tangu mwisho wa ukomunisti katika Urusi na mabadiliko katika China uchumi wa Korea Kaskazini umeporomoka. Zadi ya nusu ya viwanda vya Pyonyang vimefungwa. Umeme unapatikana kwa masaa pekee. Watazamaji kukadiria ya kwamba njaa mjini si kali kama vijijini na kwenye miji mingine kwa sababu mji mkuu hupendelezwa katika mgawanyo wa vyakula na bidhaa chache zinazopatikana.
Makala hiyo kuhusu "Pyonyang" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Pyonyang kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |