Roma ya Kale
From Wikipedia
Roma ya Kale ni ustaarabu uliokua kutoka katika mji na taifa la Roma, ulioanzishwa katika rasi ya Kiitaliano katika karne ya 9 KK. Katika kipindi cha karne kumi na mbili cha uhai wake, ustaarabu wa Roma ulibadilika toka kuwa dola, hadi kuwa jamhuri ya wachache wenye nguvu, na hadi kuwa ufalme mkubwa. Roma ya Kale ilikuja kutawala Ulaya Magharibi na eneo zima linalozunguka bahari ya Mediteraneo kupitia mapambano na kuungana. Hata hivyo, sababu kadhaa zilisababisha hatimaye kuanguka kwa ufalme wa Roma. Sehemu ya magharibi ya ufalme, ukijumuisha Uhispania, Gaulia na Italia, hatimaye ilijiengua na kuwa dola huru katika karne ya tano; sehemu ya mashariki ya ufalme iliyoongozwa toka Constatinopo, ndiyo iitwayo Ufalme wa Byzantini baada ya mwaka 476 BK, tarehe ya kitamaduni ya “kuanguka kwa Roma” na hatimaye mwanzo wa Zama za Kati.