Sekundi
From Wikipedia
Sekundi (alama: s; pia: sekunde, nukta) ni kipimo cha wakati na kati ya vipimo vya kimsingi wa SI.
Kiasili ilihesabiwa kama sehemu ya 60 ya dakika moja lakini kisayansi inapimwa sasa kulingana na mwendo wa mnurulisho wa atomi za sizi -133.
Sekundi 60 ni dakika moja, na sekundi 3,600 ni saa moja.
Kisasili siku iligawiwa kwa masaa, masaa kwa dakika na dakika kwa sekundi. Imeonekana ya kwamba hesabu hii haitoshi kwa matumizi ya kisayansi kwa sababu muda wa siku si sawa kamili kutokana na mwendo wa dunia yetu. Hivyo kipimo kamili cha sekundi ilitafutwa kinachopimika katika fizikia na sasa muda wa vipimo vingine vya wakati inahesabiwa kwenye msingi wa sekundi siyo kinyume. Tokeo mojawapo ni ya kwamba siku hailingani tena kamili na masaa 24.
Makala hiyo kuhusu "Sekundi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Sekundi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |