Vipimo sanifu vya kimataifa
From Wikipedia
Vipimo sanifu vya kimataifa (Kifar.: Système International d'unités; kifupi chake: SI) ni utaratibu uliokubaliwa kimataifa kwa kuwa na vipimo vya pamoja duniani. Maendeleo na matumizi ya utaratibu huo huangaliwa na Ofisi ya Kimataifa ya Vipimo.
Msingi wa utaratibu huu ni mita. Vipimo vingine ni vya urefu (mita), masi (kilogramu), wakati (sekondi), mkondo wa umeme (ampea), halijoto (kelvini), kiasi cha dutu (moli), mwangaza au ukalifu nunurikaji (kandela).
Vipimo hivi hutumika na wanasayansi duniani. Katika maisha ya kawaida kuna vipimo mbalimbali vinavyoweza kuwa tofauti kati ya nchi na nchi.