Wolfgang Amadeus Mozart
From Wikipedia
Wolfgang Amadeus Mozart (aliyebatizwa Joannes Chrysostomus Wolfgangus Theophilus Mozart; 27 Januari, 1756 – 5 Desemba, 1791) ni mwandishi wa muziki muhimu na kupendwa kwa muda mrefu, wa muziki ya klasiki ya Ulaya. Mazao yake makubwa sana yanazingatia nyimbo ambazo hutambuliwa kuwa vilele vya muziki ya sinfoni, vikundi vidogo, piano, opera, na kwaya. Nyimbo nyingi zake ni sehemu ya kawaida ya maonyesho ya muziki, na ni maarufu kama kazi bora ya mtindo wa klasiki.