Abu Dhabi
From Wikipedia
Abu Dhabi (Kiarabu: أبو ظبي ʼAbū Ẓaby) ni ufalme mkubwa katika Shirikisho la Falme za Kiarabu kwenye rasi ya Uarabuni na pia jina la mji mkuu wa ufalme huu.
Mji wa Abu Dhabi ni mji mkuu wa shirikisho. Mwaka 2000 palikuwa na wakazi wapatao 1,000,000. Mji umejengwa kwenye kisiwa karibu na mwambao. Takriban 80% za wakazi si wazalendo bali wageni.
Hadi 1970 ilikuwa mji mdogo wa nyumba za matofali ya matope. Tangu kupatikana kwa pesa ya mafuta mji ulikua kupita kiasi na nyumba zote ni mpya. Maji matamu hutengenezwa kutokana na maji ya chumvi ya bahari. Wakazi walio wengi sana si tena wazalendo bali wageni hasa kutoka Asia ya Kusini.
Kuna mji wa pili katika ufalme ni Al Ain yenye wakazi 348,000 (2003 sensa). Mji wa Ruwais ulianzishwa jangwani kabisa.