Bara
From Wikipedia
Bara (au kontinenti) ni sehemu kubwa ya ardhi iliyochomoza juu ya bahari, ambayo kikawaida hukaliwa na watu na kuwa juu yake milima na mimea na wanyama na kila aina ya viumbe. Sehemu hii ya ardhi ndio inayojulikana kama bara, na sehemu nyengine ya ardhi ni ile iliyoko chini ya bahari.
Kwa kawaida huhesabiwa katika dunia mabara saba, mengine yakiwa makubwa na mengine madogo.
- Bara la Afrika
- Bara la Asia
- Bara la Amerika ya Kaskazini
- Bara la Amerika ya Kusini
- Bara la Antaktika
- Bara la Ulaya
- Bara la Australia
Mara nyingi visiwa vya Pasifiki hujumlisha pamoja na Australia kama
na kuhesabiwa kama bara.
Kuna mahesabu tofauti yanayojumuisha Amerika ya Kaskazini na Amerika Kusini kuwa bara moja, au Ulaya na Asia kuwa bara moja la Eurasia.
[edit] Eneo la Mabara ya Dunia
Kuna katika ulimwengu wetu huu, mabara saba (7): Asia, Afrika, Amerika ya Kaskazini na ya Kusini, Antaktika, Australia na Ulaya (Uropa). Eneo la mabara haya ni kama ifuatavyo, kuanzia na kubwa kabisa hadi dogo kabisa.
- Bara la Asia lina eneo la 44,579,000 kilomita mraba.
- Bara la Afrika lina eneo la 30,065,000 kilomita mraba.
- Bara la Amerika lina eneo la 42,075,000 kilomita mraba.
- Bara la Antaktika lina eneo la 13,209,000 kilomita mraba.
- Bara la Australia lina eneo la 7,687,000 kilomita mraba.
- Bara la Uropa au Ulaya lina eneo la 9,938,000 kilomita mraba.
[edit] Eneo la dunia
Eneo la ardhi yote kwa jumla ni [510,066,000 kilomita mraba], ikiwa nchi kavu imechukuwa eneo la [148,647,000 kilomita mraba] na maji yamechukuwa eneo la [361,419,000 kilomita mraba]. Eneo la maji kulingana na eneo la nchi kavu ni asilimia 70.9, na nchi kavu [148,647,000 kilomita mraba] ni asilimia 29.1. Maji ya bahari yamechukuwa eneo la [335,258,000 kilomita mraba]ambalo ni asilimia 97, na maji yaliyobakia matamu ni asilimia 3 tu.
[edit] Nchi za Mabara haya
- Bara la Asia lina nchi huru 44.
- Bara la Afrika lina nchi huru 53.
- Bara la Amerika ya kaskazini lina nchi huru 35.
- Bara la Antaktika halina wakazi wa kudumu wala nchi huru hata moja ijapokuwa nchi kama 7 zinadai kumiliki sehemu fulani za bara hili.
- Bara la Australia au Oshania lina nchi huru 14.
- Bara la Ulaya (au Uropa) lina nchi huru 46.
Kwa hivyo, kwa ujumla, kuna madola 192 katika mabara yote ya ulimwengu, mara huzidi kukitokea na mgawanyiko wa nchi au hupungua kukitokea umoja au muungano wa nchi.