Australia
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: (hakuna) | |||||
Wimbo wa taifa: Advance Australia Fair Wimbo la kifalme: God Save the Queen |
|||||
Mji mkuu | Canberra |
||||
Mji mkubwa nchini | Sydney | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza (hali halisi, si kisheria)1 | ||||
Serikali
1: Malkia wa Australia,
2: Gavana Mkuu, 3: Waziri Mkuu |
Shirikisho la kifalme 1: Elizabeth II wa Uingereza, 2: Michael Jeffery, 3: John Howard |
||||
Uhuru Katiba ya Australia |
1.1. 1901 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
7,741,220 km² (ya 6) 1 |
||||
Idadi ya watu - 2006 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
20,555,300 (53rd) 18,972,350 2.6/km² (224th) |
||||
Fedha | Australian dollar (AUD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
various2 (UTC+8–+10) various2 (UTC+8–+11) |
||||
Intaneti TLD | .au | ||||
Kodi ya simu | +61 |
||||
1English does not have de jure official status (source) 2There are some minor variations from these three time zones, see Time in Australia |
Australia ni bara pia ni nchi. Iko kusini ya Indonesia na magharibi ya New Zealand. Ikiwa na eneo la 7.682.300 km² ni bara ndogo kabisa duniani, kama nchi ni nchi kubwa ya sita. Mara nyingi visiwa vya New Zealand huhesabiwa kuwa sehemu ya bara la Australia. Vilevile Australia huangaliwa pamoja na visiwa vya Pasifiki katika orodha la mabara ya dunia kama "Australia na Pasifiki".
Australia huzungukwa na bahari ya Hindi, bahari ya Pasifiki na Bahari ya Kusini.
Idadi ya wakazi ni milioni 20 (mwaka 2004).
[edit] Ekolojia
Australia ilitengwa na mabara mengine miaka milioni mingi iliyopita. Kwa sababu hiyo kuna aina nyingi za pekee za mimea na wanyama zisizopatikana penginepo duniani. Wanyama wa pekee ni kwa mfano kanguru na koala. Miti ya Australia kama vile mkalitusi imepelekwa kote duniani katika nchi zenye hali ya hewa ya kufaa.
[edit] Historia
Watu wa kwanza walifika Australia takriban miaka 50,000 iliyopita. Walitunza utamaduni wa wavindaji-wakusanyaji hadi kufika kwa ukoloni.
Hakuna habari kama watu wa Asia walifikia Australia lakini tangu karne ya 17 BK Waholanzi halafu Waingereza walifika kwa jahazi zao.
Australia ikawa mahali pa koloni ya kigereza na wafungwa kutoka Uingereza walipelekwa hapa katika karne ya 19 BK. Baadaye walifika pia walowezi huru.
Idadi ya Waustralia asilia imepungua sana kutokana na magonjwa mapya wakiambukizwa na Wazungu pia wametendewa vibaya na kufukuzwa katika sehemu kubwa ya nchi yao.
Australia ilipata uhuru wake mwaka 1901 lakini inaendelea kumkubali malkia ya Uingereza kama Mkuu wa Dola akiwasilishwa na Gavana Mkuu. Mamlaka iko mkononii wa waziri mkuu na serikali yake.
[edit] Serikali
Muundo wa utawala ni ya shirikisho. Kuina majimbo 6 ya kujitawala pamoja na maeneo ambayo ni moja kwa moja chini ya serikali ya shirikisho.