Bendera ya Msumbiji
From Wikipedia
Bendera ya Msumbiji ina milia mitatu ya kulala ya rangi kijani - nyeusi - njano. Mlia mweusi ulio katikati ina kanda mbili nyembamba byeupa kando. Upande wa nguzo kuna pembetatu nyekundu yenye jembe, bunduki na kitabu juu ya nyota njano ndani yake.
Bendera hii ilikubaliwa mwaka 1983. Msingi wake ni bendera ya chama cha FRELIMO iliyofuata mfano wa bendera ya ANC ya Afrika Kusini.
Tangu mwaka 2005 kulikuwa na maandalizi ya kupata bendera mpya lakini haijakubaliwa hadi 2006.
Hasa picha ya bunduki aina AK-47 imekumbusha wananchi wengi kuhusu siku za vita ya wenyewe wa wenyewe baada ya kupata uhuru wakupendelea kutokuwa na picha hiyo. Lakini wengine wanaiona kama kumbukumbu ya mapambano ya ukombozi.
Bendera inatumia rangi za Ethiopia au rangi za Umoja wa Afrika ambazo ni kijani - njano - nyekundu.
[edit] Maana ya rangi
Mara nyingi maana zifuatazo zinatolewa kwa ajili ya maana ya rangi:
Kijani: Utajiri wa ardhi
Nyeusi: Bara la Afrika
Njano: Utajiri wa madini
Nyeupe: Amani
Nyekundu: Mapambano ya uhuru
Nembo:
Nyota njano: Kushikamana pamoja kwa wananchi
Kitabu: Elimu
Jembe: Kilimo
AK-47: Nia ya kutetea uhuru