Brussels
From Wikipedia
Brussels (Kifaransa: Bruxelles, Kijerumani: Brüssel) ni mji mkuu wa Ubelgiji na pia makao makuu ya ofisi za Umoja wa Ulaya.
Kisheria jina la Brussel inataja mambo mbalimbali:
- mji wa Brussel mwenye wakazi 142,000 kwenye eneo la 32 km².
- Jimbo la Brussel ambamo mji wa Brussels pamoja na miji 18 mingine inayojitawala ni sehemu moja tu. Sehemu hizi zote ni hali halisi kama mji mmoja mkubwa lakini kisheria kila sehemu bado ina hali yake ya pekee. Jimbo lina wakazi milioni moja. Cheo cha mji mkuu kinamaanisha jimbo lote si mji pekee yake.
Mji umejulikana tangu mwaka 966 BK lakini kuna uwezekano ya kwamba umri wake ni mkubwa. Katika karne ya 15 BK ulikuwa mji mkuu wa utemi wa Brabant ukitajirika kutokana na karahana zake za nguo na biashara yake. Baadaye Brussel pamoja na Ubelgiji ilikuwa chini ya watawala wa nje kwanza Hispania halafu Uholanzi. Mapinduzi wa 1830 yalileta uhuru na Brussel ikawa mji mkuu wa taifa jipya katika Ulaya. Katika karne ya 19 mji uilikua sana katika mapinduzi ya viwandani.
Tangu 1958 Brussel imekuwa mji mkuu wa Ulaya kwa sababu imeteuliwa kuwa makao makuu ya ofisi za Umoja wa Ulaya - wakati ule mtangulizi wake Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya. 1967 makao makuu ya NATO yalifuata ikahamia baada ya fitina kati ya Marekani na Ufaransa.
Kati ya majengo maarufu sana za Brussel ni Atomium iliyosimamishwa wakati wa Maonyesho ya Dunia 1958.