Ernst Ruska
From Wikipedia
Ernst August Friedrich Ruska (25 Desemba, 1906 – 27 Mei, 1988) alikuwa fundisanifu wa umeme kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa anajulikana kwa kubuni hadubini ya elektroni. Mwaka wa 1986, pamoja na Gerd Binnig na Heinrich Rohrer alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.