Frederick Banting
From Wikipedia
Frederick Grant Banting (14 Novemba, 1891 – 21 Februari, 1941) alikuwa daktari kutoka nchi ya Kanada. Hasa alichunguza ugonjwa wa usukari, na pamoja na Charles Best aligundua dawa ya insulini. Mwaka wa 1923, pamoja na John Macleod alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba. Mwaka wa 1934 alipewa cheo cha “Sir” cha Uingereza.