Haiti
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: L'Union Fait La Force ("Umoja ni nguvu") |
|||||
Wimbo wa taifa: La Dessalinienne | |||||
Mji mkuu | Port-au-Prince |
||||
Mji mkubwa nchini | Port-au-Prince | ||||
Lugha rasmi | Kifaransa and Kikreoli cha haiti, Kihispania (si rasmi) | ||||
Serikali
Rais
Waziri Mkuu |
Jamhuri René Préval Jacques-Edouard Alexis |
||||
Uhuru kutoka Ufaransa |
1 Januari 1804 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
27,750 km² (ya 147) 0.7 |
||||
Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - 1982 sensa - Msongamano wa watu |
8,528,0001 (ya 88) 5,053,792 292.7/km² (ya 39) |
||||
Fedha | Gourde (HTG ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-5) (UTC-4) |
||||
Intaneti TLD | .ht | ||||
Kodi ya simu | +509 |
Haiti ni nchi kwenye kisiwa cha Karibi cha Hispaniola. Mji mkuu ni Port-au-Prince. Eneo la Haiti ni takriban theluthi moja ya Hispaniola yote. Sehemu nyingine ya kisiwa ni nchi jirani ya Jamhuri ya Dominika.
Haiti ni nchi ya kwanza duniani ambako watumwa Waafrika walifaulu kupindua utumwa na kujipatia uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1804.
Jina la "Haiti" lina asili katika lugha ya Kitaino ya wakazi asilia lamaanisha "nchi ya milima" na ni kweli kisiwa pama milima mingi. Haiti ni kati ya nchi maskini kabisa duniani na nchi maskini zaidi Amerika kote.
Nchi ina wilaya kumik. Kuna lugha rasmi mbili moja ni Kifaransa na nyingine Kikreoli ya Haiti ("Kweyol"). Wakazi wengi ni Wakristo wakatoliki lakini wengi hufuata vilevile dini ya vudu inayotoka na imani za jadi kutoka Afrika ya Magharibi.
Contents |
[edit] Historia
[edit] Mianzo na ukoloni wa Hispania
Wakazi asilia walikuwa Waindio Waarawak. Baada ya kufika kwa Kristoforo Kolumbus na utawala wa Hispania idadi yao ilipungua haraka kutokana na magonjwa ya Ulaya ambayo hawakuzoea na kukosa kinga dhidi yao na pia kutokana kutendewa vibaya kwa unyama na mabwana wapya. Mnamo mwaka 1600 Waindio wachache tu walibaki kutoka malakhi wakati wa Kolumbus wakapotea kabisa kwa njia ya kuoa au kuolewa na wazungu na weusi. Wahispania walianzisha mashamba kwa kazi ya watumwa kutoka Afrika.
[edit] Ukoloni wa Ufaransa
Katika karne ya 17 Wafaransa walifika kisiwani wakanunua theluthi moja ya kisiwa wakaiita "Saint-Domingue" kilichokuwa baadaye Haiti. Wafaransa walileta watumwa wengi kutoka Afrika na kujenga uchumi wa mashamba makubwa hasa ya miwa. Koloni ya Saint-Domingue ilikuwa koloni tajiri ya Ufaransa katika Amerika.
[edit] Mapinduzi ya Ufaransa
Wakati wa mapinduzi ya Ufaransa 1789 koloni ilikuwa na wakazi wa aina nne:
- Wazungu hasa Wafaransa waliokuwa mabwana lakini waliokuwa na tofauti kubwa kati yao wengine tajiri sana wengine maskini -jumla takriban watu 32,000
- chotara na weusi huru ambao walikuwa raia wa daraja ya pili; wengine walikuwa matajiri na mabwana wa mashamba na pia wa watumwa - jumla watu 28,000
- watumwa wa asili ya Kiafrika - jumla watu 500,000
- Wamaroni walikuwa watumwa wakimbizi walioishi mlimani katika pori - idadi yao haijulikana hawakuwa wengi.
Mapinduzi ya Ufaransa na kutangaziwa kwa haki za kibinadamu vilisababisha matumaini ya chotara wenye mali ya kukubaliwa kama raia kamili wenye haki ya kupiga kura. Wenyewe hawakutegemea kumaliza utumwa uliokuwa msingi wa uchumi. Lakini matumaini yao yalishindikana wakakataliwa na watawala kisiwani.
[edit] Mapinduzi ya Haiti
Sehemu ya matajiri kati ya Wazungu walitaka kujitenga na Ufaransa kwa msaada wa Uingereza na Hispania wakichukia mapinduzi katika Ufaransa. Watumwa na weusi huru wenye elimu walifuata habari hizi wakaogopa ya kwamba utawala wa mabwana hawa bila sheria za Ufaransa uatkuwa vibaya zaidi kuliko hali jinsi ilivyokuwa wakaanza mapinduzi.
Kiongozi wao alikuwa Toussaint L'Ouverture aliyefaulu kushika serikali ya koloni tangu 1798. Awali alipigania jeshi la Ufaransa; baada ya bunge la Paris kutangaza mwisho wa utumwa alishirikianna na Ufaransa dhidi ya jeshi la mabwana wenye shamba waliotaka kuendeleza utumwa katika nchi ya kujitegemea.
Toussaint L'Ouverture alishinda pia Waingereza waliotaka kuwasaidia wapinzani Wafaransa wa Paris na 1801 akateka kaskazini ya kisiwa iliyokuwa eneo la Kihispania na kutawala Hispaniola yote akitangaza kote mwisho wa utumwa.
Lakini mmnamo mwaka 1802 siasa ya Paris ilibadilika na mtawala Napoleon Bonaparte aliamua kurudisha Hispaniola kwa hali ya awali akatuma jeshi kubwa la askari 40,000. L'Ouverture alikamatwa alipokubali kushauriana na jenerali Mfaransa akapelekwa kama mfungwa Ulaya. Lakini makamu wake Jean-Jacques Dessalines aliposikia khusu mipango ya Ufaransa ya kurudisha utumwa alianza vita upya. Katika vita vikali Wafaransa walishindwa na Dessalines alitangaza uhuru wa koloni tarehe 1 Januari 1804 kwa jina la "Haiti" kama "Jamhuri ya watu weusi".
Makala hiyo kuhusu "Haiti" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Haiti kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |