Ikweta
From Wikipedia
Ikweta ni mstari unaogawa dunia katika sehemu mbili (kaskazini na kusini) kwenye umbali sawa kati ya ncha ya kaskazini na ya kusini.
Baina ya nchi za Afrika ni Somalia, Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kongo, Gaboni na Sao Tome na Principe ambazo ziko kwenye mstari wa ikweta.
Katika Amerika ikweta inapita Ekwado (jina limetokana na neno la ikweta kwa Kihispania), Kolombia na Brazili. Katika Asia ikweta inapita funguvisiwa ya Indonesia.
Makala hiyo kuhusu "Ikweta" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Ikweta kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |